Wakati macho na masikio ya dunia yote yakiwa kwenye soka hasa kwa
kipindi hiki cha kombe la dunia sasa inshu imekuwa tofauti kwa kampuni
ya Beats by Dr.Dre ambayo headphone zake zimepigwa marufuku kutumika
kwenye kombe la dunia.
kampuni ya Beats Electronics ilitoa tangazo la luninga lililokuwa na
dakika 5 ambalo walilipa jina la ‘Tittle the Game before the Game’.
Katika tangazo hilo wapo mastar kadhaa wa mpira wa miguu kwa msimu
huu akiwemo mchezaji nyota toka Brazil Neymar Da Silva Santos
Júnior,Mchezaji wa Spain Francesc “Cesc” Fàbregas pamoja na mchezaji
kutoka Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz pamoja na Lil Wyne.
Unaambiwa baada ya FIFA kuliona hilo tangazo wamewakataza wachezaji
wote kuvaa headphones hizo za Beats by Dre wakiwa kwenye viwanja hivyo
vya kombe la dunia pamoja na sehemu zote za sherehe zitakazowahusisha
pia waandishi.
Dili limeidondokea kampuni ya Sony ambao ni Official Partner na FIFA
ambao wameahidi kuwapatia wachezaji hao headphones za kuvaa kwa kipindi
hicho cha kombe la Dunia na hawataruhusiwa kuvaa aina nyingine yoyote ya
headphone
Thank you for taking your time to find out more about the blog. This blog is your number one event, sports, advertisement and entertainment news. Welcome to an Entertainment revolution. Advertisement gate way and promotion as well, STAY ON IT ENJOY CALL / SMS +255 686 123425 for more information and any blog assistance
Wednesday, 18 June 2014
HEADPHONE ZA DR, DRE ZAKATALIWA WORD CUP

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment