Friday, 19 October 2012

YANGA YASHINDA KAMPENI YAKE NA VODACOM KUHUSU KUVAA JEZI NYEKUNDU, SASA WAPEWA RANGI WANAYOTAKA


Kampuni ya simu za mkononi Vodacom ambao pia ni wadhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wamefikia muafaka na klabu ya Yanga juu ya kutotumia jezi zenye nembo nyekundu.
Vodacom imefikia hatua hiyo kutokana na Yanga kupeleka maombi yao ya kuomba kutotumia nembo hiyo nyekundu katika jezi zao, vodacom imeona ni busara kuwasikiliza Yanga hivyo kuamua kuipa nafasi ya kuchagua nembo moja kati ya hizo tatu hapo juu, klabu ya Yanga imawahakikishia washabiki wake kuwa hawatakubali kutumia rangi yeyote nyekundu katika jezi zao au kitu chochote kitakachokuwa kikitumiwa na klabu iyo kwa ni DHAMBI kwao, Kampuni ya Vodacom imetoa nembo tatu tofauti ili kuweza kuwaruhusu yangu kutumia moja ya nembo watakayokuwa wamapendezewa nayo,

No comments: