Sunday, 14 April 2013

YANGA BASI TENA, AKUNA KAMA YANGA

Dar es salam Young Africans wameukaribia ubingwa wa Ligi kuu ya soka ya Tanzania bara inayodhaminiwa na Vodacom Tz Ltd baada ya kuondoka na pointi kwenye mchezo dhidi ya timu ya Jkt Oljoro toka Arusha kwa mabao matatu bila (3-0).
Ushindi huo wa Yanga ulipatikana baada ya mabao ya mshambuliaji wa Uganda Hamis Kiiza ‘Diego’ , kiungo wa Taifa Stars Frank Damayo na winga ambaye pia aliwahi kuwa Dancer wa THT Simon Msuva ambapo ushindi huo unawafanya Yanga wafikishe pointi 51 wakiwa wanaizidi Azam Fc kwa pointi sita huku ikiwa imebaki michezo minne kabla ya ligi kumalizika.
Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kushinda mchezo kwa idadi kubwa ya mabao baada ya kushuhudia timu hiyo ikishinda mechi nyingi kwa idadi ndogo ya magoli hali iliyoonekana kumkera kocha Mdachi Ernst Brandts


No comments: