Sunday, 14 April 2013

PIGO KWA LOS ANGELES LAKERS

Timu ya Los Angeles Lakers ambayo iko kwenye mapambano makali ya kusaka nafasi ya kucheza hatua za mtoano kwenye ligi ya NBA imepata pigo kubwa ambalo huenda likaiathiri timu hiyo kimatokeo baada ya nyota wake na mchezaji bora ambaye ameibeba Lakers kwenye karibu kila mechi ya msimu huu Kobe Bryant kupata jeraha litakalomfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita hadi tisa.
Kobe alionekana kuchechemea kuelekea mwishoni mwa mchezo wa Lakers na Golden State Warriors ambapo Lakers walishinda kwa pointi 116-118 huku Kobe mwenyewe akifunga pointi 34 . Awali ilidhaniwa kuwa ni jeraha la enka ambalo limekuwa likimsumbua star huyo kwa muda mrefu lakini vipimo vilivyofanywa na madaktari wa timu hiyo vilithibititisha kuwa jeraha hilo ni kubwa na lilihitaji upasuaji.Tayari Kobe Bryant amefanyiwa upasuaji uliofanywa siku ya jumamosi ambao inataarifiwa kuwa umeenda vizuri chini ya madaktari bingwa wa masuala ya majeraha ya wachezaji wa NBA Dr.Neal El Attrache na Dr Stephen Lombardo lakini taarifa mbaya kwa mashabiki wa Lakers ni kwamba nyot huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita mpaka tisa kabla ya kurejea akiwa fit, Lakers inapambana na timu ya Utah Jazz kusaka nafasi ya nane na ya mwisho kufuzu hatua za mtoano ya NBA PLAY OFFS kwa kanda ya magharibi huku ikiwa imesalia michezo mitatu kwa hatua ya mzunguko ya ligi hiyo kumalizika .Bryant amekuwa akiibeba Lakers kwa uwezo wake binafsi na jeraha alilolipata linaweza kuathiri timu hiyo kwenye michezo yake mitatu iliyosalia au hata ya mbeleni endapi watafuzu hatua ya mtoano.Hali hii itawalazimu wachezaji wengine wa Lakers kupambana kufa na kupona kuhakikisha wanafuzu hatuaya mtoano na huenda wakafanikiwa kufanya hivyo bila Kobe kama ilivyokuwa kwa Boston Celtics ambao wamepambana kuhakikisha wanafuzu bila ya nyota wake Rajon Rondo ambaye aliumia mapema mwanzoni mwa msimu na kukaa nje msimu mzima

No comments: