2] Alifunga goli lake la 100 kwenye maisha yake ya soka tarehe 5 February 2012, ilikuwa siku yake ya kuzaliwa na alikuwa anafikisha miaka 20.
3] Real Madrid walitaka kumsajili toka akiwa na miaka 14,walifatilia maisha yake ya soka mpaka kumpa dili,Neymar alipitia mambo yote mpaka vipimo vya afya ila mwaka 2011 ilishindikana kwenda Real pale Santos walipotoa pesa nyingi zaidi kumbakiza Brazil.
4] West Ham ndio klabu kubwa ya kwanza kutaka kumsajili Neymar baada ya kuona kipaji chake, Ilikuwa tayari kutoa paundi milioni 12, ndio chanzo cha Neymar kutambulika kama mchezaji wa kimataifa zaidid,ikafwatiwa na Chelsea.
5] Neymar alikosa namba kwenye kikosi
cha timu ya taifa ya brazil ya kombe la dunia la mwaka 2010
kilichopangwa na Dunga, hakuwepo hata kwenye wachezaji wa dharura ingawa
Pele na Romario walipendekeza awepo.
6] Neymar amekuwa baba akiwa na miaka
19,mtoto wake wa kwanza wa kiume anaitwa David Lucca na mpaka sasa
Neymar hajaijulisha dunia mama wa mtoto ni nani.
7] Neymar ni mchezaji wa tisa kwenye
orodha wa wachezaji wa Barcelona walionunuliwa kwa ada kubwa zaidi. Ada
yake ya uhamisho ni €57 million.
8] Ukizingatia wachezaji wakali
wanaotoka Brazil, Neymar ndio mchezaji wa kwanza wa Brazil kukava jarida
la Time, Na Wabrazil wengi waliokava jarida hili ni wanasiasa.
9] Neymar alivyojiunga na Barcelona
alipewa dili linalomlipa dola milioni 74 ndani ya mwaka mmoja, mwaka
2012 alitajwa kuwa mchezaji wa saba tajiri zaidi duniani huku jarida la
Forbes likimtaja kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani mwenye miaka
chini ya 25. Kwa sasa ni wa sita kwenye wanasoka na wanamichezo matajiri
zaidi duniani.
10] Mwaka 2012 na 2013 Neymar ametajwa
kuwa mchezaji anayeuza zaidi akiwekwa kwenye matangazo na Jarida la
SportsPro na kuwafunika wachezaji kama Ronaldo, Messi,Rory McLlroy na
Usain Bolt.
No comments:
Post a Comment