Mabaki ya miili ya watu zaidi ya 100 imekutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji, kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yalionekana jana katika eneo hilo majira ya jioni na kuvuta mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia tukio hilo.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema , mabaki yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Alisema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa.
Alisema waliobaini kuwapo kwa mabaki hayo ni majirani wa eneo hilo ambao walitoa taarifa polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alipoulizwa alisema wakati huo alikuwa eneo la tukio na kwamba angetoa taarifa baadaye
Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa.
Mabaki hayo ya miili yameonekakana kuvuta mamia ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo,baadhi ya mashuhuda walipoulizwa wamesema mabaki hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika mifuko ya plastiki ikiwa imefungwa juu.
Wameongeza kwa kusema mabaki hayo ambayo yamekaushwa na kuhifadhiwa katika mifuko ya ujazo wa kilo 25 ni pamoja na miguu, mikono, mbavu na mafuvu ya vichwa hata hivyo Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuanza kupakia mabaki hayo katika gari lao lenye namba za usajili MS 54 UKH na kuipeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment