Tuesday, 7 January 2014

DIAMOND FOREVER - KAMA ULIKOSA MARA YA KWANZA , BASI MWAKA HUU UNAKUHUSU PALE PALE KUTOKA KWA YULE YULE

Kwa mara ya kwanza ilifanyika pale Mlimani City na kiingilio kilikuwa ni elfu hamsini za kitanzania ikiwa imebeba title ya ‘Diamonds Forever’.
Naseeb Ablul maarufu kama Diamond Platnumz ameweka wazi juu ya kufanyika kwa mara nyingine show ya namna hiyo jijini Dar siku ya wapendanao duniani yaani tarehe 14/2/2014. Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha redio Clouds FM kupitia kipindi cha XXL, Diamond alifunguka juu ya show hiyo kutofanyika mwaka jana na kufanyika mwaka huu..
“Kwa kweli tulipanga mwaka jana tufanye show ya Diamond Forever lakini kutokana na ratiba kuingiliana tulishindwa kufanya hivyo ila shughuli kubwa ilikuwa ni kutafuta chaneli za mziki wa Bongo Fleva nje ya Tanzania. Mwaka huu tumepanga kufanya siku ya wapendanao yaani Valentine day.” – Diamond.
Baabkubwa inamtakia kila la kheri katika kufanikisha jambo hili..

No comments: