Saturday, 22 December 2012

HIKI NDIO ALICHOANDIKA DJ CHOKA KATIKA UKURASA WAKE WA FACEBOOK KUHUSU WATANGAZAJI WA BONGO NA MEDIA ZAO

Naomba niseme hivi..kuna watoto wameingia kwenye hii fani ya utangazaji na wanajiona wako juuuuuu sana bila kukumbuka hapo walipo ni hiyo media wanayofanya kazi ndio inawabeba...sasa basi kama upo kwenye hiyo sehemu na ukaona umepata jina basi usinitumie mimi kama condom kisha ukanifua na kunitumia tena. Huu mziki wa bongo umekuwa wakuendeshwa endeshwa na watu fulani ambao wanadhani wameshafika levo ya kuongea na msanii mkubwa kwa dharau au kwa kusema unampa promo. Nachokuomba ww mtanazaji wa radio fulani hapa bongo heshimu kile ninachokifanya na usione kama nimelingana na ww au unaendesha gari now days ndio uongee na me kama naongea na Mungu. Kama unasema bila ww djchoka apati promo basi brand yangu mimi ilishatengenezwaga kitambo na Profesa Jay sasa hivi inapigwa msasa na siwezi kuwa na majivuno coz najua kuna siku nitakufa na nitauacha huu mziki coz mziki hauna mwenyewe. NIMEMALIZA

No comments: