Tuesday, 27 November 2012

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEIN - SHARO MILIONEA

Mungu ndo muweza wa yote na hakika kila alipangalo akuna mwenye uwezo wa kupangua, leo upo mbele yetu kesho tutakuwa pamoja my brother , niliheshimu kazi zako na kuheshimu utu wsko kwangu lakini leo nasema mengine kuwa umetangulia katika haki ya milele, nilitamani niendelee kuwa na wewe lakini imekuwa tofauti kumbe mola anakuhitaji uwe ne siku zote kuliko nnavyokuhitaji mimi,

nitashindwa kufika kwenye mazishi yako kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu lakini DUA zangu kwako ndo kila kitu mbele ya mola kwani adhabu za kaburi zilianza pindi mola alipokuchukua, Leo umeende na kesho ntakufuata kaka yangu,

ilikuwa jumatatu iliyoanza na furaha kubwa sana kwangu lakini siku ilipokuwa inakaribia kuisha ilibadilika na kuwa siku ya huzuni,  nilipokea simu kutoka kwa Rafiki yangu wa karibu ambaye pia ni mwanamuziki mkubwa wa mionoko ya bongo fleva kuwa kuna taarifa za ajali ya gari maeneo ya muheza linamuhusisha sharo milionea, ilikuwa nhgumu kuamini kuwa umekenda japokuwa tuliwasiliana siku moja kabla na kuongea mipango ya biashsra na nilipojaribu kuuliza kwa watu wako wa karibu pia walikuwa hawana iyo taarifa ndipo nilipopiga simu kwa watu walipo maeneo ya tanga na kuuliza kuwepo kwa taarifa izo za ajali na kunithibitishia kuwa ni kweli na mwanamuziki na maigizo ya vichekesho sharo milionea husseun mkiety atunae tena,  sikuamini na siku ilbadilika kuanzia hapo na kufanya iwe mabaya sana na mpaka naandika habari hii bado sijui nini kitaendelea baada ya kutuacha, mbele wewe nyuma sisi sharo milionea.

UMEENDA KAKA, KESHO NITAKUWA NAWE
MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEIN


No comments: