Friday, 19 October 2012

ZANZIBAR BADO HALI SI SHWARI

Mpaka sasa hivi hali katika baadhi ya vitongoji visiwani Zanzibar sio shwari pamoja na kwamba serikali imetoa tamko kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Vurugu zilianza toka jana kutokana na kukamatwa kwa kiongozi wa taasisi ya kiislamu, Sheikh Farid Hadi Ahmed ambapo msemaji wa polisi Znz Mohamed Mhina amesema mpaka leo wafuasi wa kikundi cha Uamsho wameendelea na vurugu na uchomaji wa matairi barabarani na kuweka mawe.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba leo ndio imethibitishwa kuuwawa kwa askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU Saidi Abdul-Rahman, ameuwawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Pamoja na watu waliofanya tukio hilo kutofahamika msemaji wa polisi Mhina amesema wanaosadikiwa kufanya hilo tukio ni wafuasi wa kikundi cha Uamsho ambapo mwili wake imepatikana na imefanyiwa uchunguzi kwenye hospitali kuu ya mnazi mmoja.
Mpaka sasa watu 10 wamekamatwa kutokana na fujo hizo vilevile Polisi wanaendelea kutafuta mahali alipo kiongozi wa kikundi cha Uamsho ambae alidaiwa kupotea tangu juzi jioni (jumanne) ambapo alimtuma dereva wake apeleke umeme nyumbani, dereva aliporudi kumfata hakumkuta.

MUNGU IBARIKI ZANZIBAR, MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments: