Monday, 22 October 2012

PHD HEMEDI KUBUNI MAVAZI YA NDANI YA WATOTO WA KIKE



Msanii wa Bongo Fleva mwenye nyota ya movie aliyekiri kuwa na mashabiki wakike zaidi anampango wa kubuni nguo za ndani za wanawake. Ubunifu huu na nguo hizi amezipa jina la `Feel Good Inside By PHD' Yani Jiskia Vizuri Ndani kwa lugha ya kiswahili.Hemedy amesema wazo la kubuni mavazi alikuwa nalo kwa muda mrefu sana na ukizingatia anapenda sana kuvaa na kupendeza so mitindo nikitu anataka kufanya kama sehemu ya kazi zake.Pia PHD amesema toka akiwa shule alikuwa mchoraji mzuri sana na ameshawahi kushinda mashindano ya kuchora akiwa shule ya sekondari. Wabunifu wengi mpaka sasa wanabuni na kutengeneza nguo za nje kama mashati na suti,Nanuku maneno machache ya Hemedy `Nachotaka kufanya kama Hemedy lazima kiwe tofauti sana na ndio maana natengeneza nguo za ndani za wanawake'.

Nguo atakazo buni na kutengeneza Hemedy ni Bra na Chupi za wanawake tu. Fahamu Kuwa nguo za ndani anazo vutiwa nazo zaidi Hemedy ni Bikini+

No comments: