ndio maana leo kwenye account yangu ya twitter nikasema, inafika kipindi sasa tuangalie, kwasababu kila mmoja anakua anamtupia lawama mwenzake na vitu vingine kama hivi, ni kwamba tukae kama wasanii kama watanzania tunaotaka tuangalie mziki huu tunataka tuupeleke wapi....
kiukweli inavyoonekana anaeuharibu mziki huu sio mtu mmoja....wasanii kama wasanii unakuta wanaandika mashairi ambayo hayaeleweki hata kwenyejukwaa perfomance zao vingine havisaidii kuupeleka mziki wetu mbali hata media inaonekana kucheza nyimbo zingine ambazo kiulweli kabisa hazisaiidii chochote kwenye mziki wetu wa Tanzania na katika harakati hizi za kuupeleka mziki wetu kwenye level, "
"lawama zangu pia nazipeleka kwa mashabiki, kwasababu wana nyimbo zao ambazo wanapioga simu wanaomba, kwenye matamasha wanasapoti ya watu wengine lakini kiukweli zile nyimbo hazisaidii chochote, mashabiki saa zingine wanaomba nyimbo ambazo hazisaidii chochote na zinakuwa mbovu, "
"lakini kitu ambacho kikubwa kabisa cha mwisho, ni kwamba serikali ina play part vipi katika swala hili, ikiwa kama baba wa watanzania wote inabidi itoe kauli,kwasababu wasanii kila siku kilio chao ni kwamba kazi zao zinaibiwa watu wanakosa ubunifu ndio maana wanaimba vitu ambavyo viko bubble gum, na vitu ambavyo havieleweki, serikali kama serikali ingejaribu kuangalia jinsi gani ya kuwasaidia wasanii wa Tanzania especially katika kazi zao, kwenye vitu kama ringtones, lakini pia katika sheria jinsi gani msanii anaweza kunufaika na kazi zake anayoifanya, kwasababu hata sasa hivi hizi stika za TRA haziwezi kusaidia kitu stika zitakuwepo lakini tatizo sugu tumeliacha, tatizo ni wizi wa kazi za wasanii......." amesema Prof Jay

No comments:
Post a Comment