MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa
wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi ameweka rekodi kwa kunyakuwa
tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama FIFA Ballon d’Or katika sherehe
zilizofanyika jijini Zurich, Switzerland. Messi mwenye umri wa miaka 25
alinyakuwa tuzo hiyo mbele ya Andres Iniesta ambaye wanacheza wote Barcelon na
mshambuliaji nyoa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.




Mwaka 2012 ulikuwa na mafanikio makubwa kwa Messi baada ya kufunga mabao mengi na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller ambaye alifunga mabao 85 huku yeye akimaliza mwaka jana akiwa amefunga mabao 91. Akishukuru mara baada ya kupokea tuzo hiyo Messi aliwashukuru waandaji na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kupiga kura ya kumchagua kubeba tuzo hiyo kwa mara ya nne.
No comments:
Post a Comment