Friday, 28 August 2015

MESSI ATWAA UCHEZAJI BORA WA ULAYA





Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona ya hispania ametangazwa kuwa mcheza bora wa ulaya kwa msimu wa mwaka 2014 / 2015 na kuwapiku mwenzake wa Barcelona na mchezaji bowa wa dunia 2013/2014 Christiano Ronaldo,

LEO MESSI amewapiku wachezaji hao wenzake kwa mbali kwa kuwa watabiri wengi walitabiri ushindi wake huo kwa kiwango kikubwa alichokionesha msimu uliopita kwa kuisadia timu yake ya taifa kufikia finali mbili za kombe la dunia na lile la copa america japokua timu yake ilipoteza finali zote mbili lakini pia ameisaidia klabu yake ya barcelona kutwaa mataji matatu kwa msimu mmoja ya la liga, copa de lay na UCL




Thursday, 6 August 2015

KOCHA MKWASA ATANGAZA KIKOSI KWA AJILI YA MAANDALIZI KUIVAA NIGERIA



Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, ambao baadaye watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 , Uturuki.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul – Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.

Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni makipa, Ally Mustafa ‘Barthez’ wa Yanga SC na Aishi Manula wa Azam FC.


Mabeki ni Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani (Yanga SC).


Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telela (Yanga SC), Abdi Banda  na Said Ndemla wote wa Simba SC.


Mawinga ni Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Simon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano na Farid Mussa (Azam FC), wakati washambuliaji ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).


Wachezaji wanaocheza nje waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mrisho Ngassa (Free State – Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – England)

BREAKING NEWS: LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI WA CUF

BREAKING NEWS: LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI WA CUF

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo na kusema atabakia kuwa mwanachama wa kawaida.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba amesema amechukua uamuzi huo kutokana na UKAWA kushindwa kusimamia makubaliano yao.

Wednesday, 5 August 2015

ANGALIA HAPA WACHEZAJI WA BARCELONA WAKIPIGA PICHA KWA AJILI YA KUANZA MSIMU MPYA WA 2015 / 2016

After the return of the squad from the United States and the appearance
of the players who took part in the recent Copa América in Chile, Luis
Enrique’s squad has taken the opportunity to complete their official
individual photographs for the season 2015/16. Some players did so prior
to the US tour and this week it

Sunday, 2 August 2015

Shilole Akiongelea ni kuhusu Baraza la sanaa Tanzania [BASATA] kumfungia...

Tazama video hapo juu Shilole akilalamika kuwa Basata hawajamtendea haki.
”Nina watu kumi nyuma yangu wana nitegemea mimi, kwa nini wasi
mchukulie hatua mwana siasa aliye mpiga mwenzake, wana kuja kunipa huku
mimi kama kama hiyo ”,.