Wednesday, 29 January 2014

CHIEF KIUMBE AELEZEA ALIVYOMPATIA GARI YAKE MPYA (Toyota Prado V8)

[Audio] Chief Kiumbe Afunguka Kuhusu Mkoko Anaomiliki Diamond Platnumz (Toyota Prado V8)
Kupitia kipindi maarufu cha Sun Rise kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha 100.5 Times Fm, kilifanikiwa kufanya mahojiano EXCLUSIVELY na Muhammed Abdallah Kiumbe, maarufu kama Chief Kiumbe kuhusiana na jinsi gani amekuwa akiwasaidia baadhi ya wasanii mbalimbali hapa nchini hasa kwenye tasnia ya muziki na kuwafanya watimize ndoto zao..Amekuwa akijipatia umaarufu kwa na kufanikisha mafanikio ya wegi kama Matonya, Q Chief, Ali Choki na wengineo.
Baada ya kubanwa sana na maswali ya waongoza kipindi hicho, Chief kiumbe alifunguka kuhusu gari (Mkoko) anaomiliki Diamond Platnumz kwa sasa, ambalo ni Toyota V8 iliyogharimu zaidi ya dola laki moja, sawasawa na milioni 245 za Kitanzania ukijumuisha na ushuru. Msikilize hapa Chief Kiumbe

No comments: