Wednesday, 13 February 2013

BREAKING NEWS : RIP BK WA WANAUME FAMILY

                                          Muasisi wa kundi maarufu wa muziki wa Bongo Flava aitwaye BARAKA MARTIN SEKELA aka BK , amefariki alfajili ya leo katika Hospitali ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa , kwa mujibu wa Hassan Isaack Umande ambaye amewahi kuwa meneja wa kundi hilo, mwili wa marehemu bado upo hospitalini hapo na familia ya marehemu inajipanga kwa mazishi. Baadhi ya Nyimbo aliwahi kuchana  ni Ndege Tunduni (verse ya kwanza), Tatu Bila, kabla ya hizo ni Sitaki Dem Rmx ya Juma Nature, Kwa Maisha alioshirikishwa na Temba  na ktk traki kali inayoitwa Tunavyoishi wakiwa na Suma Lee na Dollo.Pia marehemu amewahi kurekodi traki zake mwenyewe , bado najipanga baadaye nitaeleza zaidi
Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwao temeke maeneo ya uwanja wa taifa ambapo alipokuwa anaishi na yalipokuwa makao maku ya kundi la wanaume family kabla ya kuvunjika na kuwa katika pande mbili wanaume family na halisi ambapo BK alikuwa katika upande wa wanaume halisi akiwa na juma nature, katika picha ya hapo juu BK yupo katikati ya mwanadada na D chief au doto,

No comments: