Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia
kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki
dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions). Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim
amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu
ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la
Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu. “Itakuwa
mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili
yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco.
Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari. “Tumetoka
kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza
fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya
mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea
nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory
Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la
Dunia. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi
24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya
pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine
katika kundi hilo ni Gambia. Wachezaji
aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini
Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam),
Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga),
Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa
Sugar). Viungo ni
Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani
Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman
Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa
(Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
KILA LA KHERI TAIFA STARS
Thank you for taking your time to find out more about the blog. This blog is your number one event, sports, advertisement and entertainment news. Welcome to an Entertainment revolution. Advertisement gate way and promotion as well, STAY ON IT ENJOY CALL / SMS +255 686 123425 for more information and any blog assistance
Friday, 1 February 2013
KIM ATEUA 21 STARS WA KUIVAA CAMEROON
An Entertainer and the Owner of 60Entertainment who is near by to present TV program on local TV, Current am working with One of the Biggest company
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment