Tuesday, 8 January 2013

SOMA HAPA ALICHOKIANDIKA DJ CHOKA KUHUSU WASANII WACHANA NA BLOG YAKE

 
 


Mambo vipi wadau wote wa Bongo Star Link pamoja na wasanii wote wa bongo fleva, leo naomba nizungumze na nyie wasanii mnaochipukia na hata nyie wasanii wakubwa kwa ujumla wasanii wote mnaoimba.

Mwaka huu 2013 nimeamua kufanya kitu kimoja kizuri tu kama wewe msanii unaechipukia unataka kujulikana kwa watanzania, ningeomba sana pale uunaponitumia wimbo wako hakikisha unakuwa mzuri na sio unakurupuka na kurekodi tu bora mradi umerekodi basi unanitumia ili niweke kwenye blog.

Mwaka huu nitapokea nyimbo ambazo zimetumwa na picha ya msanii aliyeimba na wimbo uwe mzuri hapo nipo radhi kumsaidia mziki wake na sio unatuma wimbo bila picha sasa hapo nakusaidiaje watanzania wakutambue? Nitaziweka kapuni email zote ambazo nitatumiwa wimbo bila picha nzuri ambayo ina ukubwa na sio kipicha kidogooooo hata kwaliti yake haifai kukaa kwenye blog
 
 
 

No comments: